July 16, 2019


BEKI mwenye nafasi kubwa ya kupewa unahodha wa Yanga msimu ujao, Kelvin Yondani amekiri kwamba kikosi hicho kimesheheni.

Mchezaji huyo wa zamani wa Simba, alisema ana uhakika kwamba timu hiyo itacheza soka la kueleweka sasa kutokana na kusajili mafundi wanaojua. 

Lakini amekiri kwamba kwenye nafasi yake kuna ushindani mkubwa kutokana na idadi kubwa ya wachezaji waliosajiliwa lakini hajawahi kufeli wala kuhofia ushindani.

Amekwenda mbali zaidi kwa kutoa mfano wa timu ya taifa ambao huitwa wachezaji wengi na baadaye yeye kupenya katika kikosi cha kwanza kiulaini kutokana na vigezo vya makocha.

Yondani ambaye atapambana na mastaa kama Ally Mtoni ‘Sonso’ aliyetokea Lipuli, Mrundi Mustapha Suleiman aliyetokea APR ya Rwanda, Mghana Lamine Moro na Andrew Vicent ‘Dante’.

 Yondani amesema kwake yeye hana shaka na suala la kukosa namba ndani ya kikosi hicho kwani uwepo wake tu Yanga unatosha sana kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri iwe kwa mawazo au kwa kucheza.

“Katika maisha yangu ya soka siyo mara ya kwanza leo kukutana na mabeki wengi na wazuri, hata ndani ya timu ya taifa huwa wanaitwa mabeki zaidi ya watano au sita wa katikati lakini mwisho wa siku wanaotakiwa kuanza huwa ni wawili katikati na wawili pembeni,” alisema Yondani ambaye ana mjengo Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

“Jambo kubwa kwangu ni kuhakikisha nafanya mazoezi bila kuwa nini kitatokea kwani niko tayari kwa kuisaidia Yanga kwa namna yoyote ile, kocha yeye ndiye anayeweza kuamua yupi aanze na yupi asubirie lakini mwisho wa siku kila uwepo wa mchezaji kati yetu una umuhimu wake,” alisema Yondani ambaye ni beki tegemeo Taifa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic