July 8, 2019

MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo amesema kuwa harudi Bongo mpaka akaione familia.

Congo imetolewa na Madagascar kwenye michuano ya Afcon hatua ya 16 bora baada ya kupoteza mchezo kwa kufungwa kwa penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya mabao 2-2.

"Tumetolewa kwa penalti hiyo si mbaya sasa ni muda wangu wa kwenda Ulaya kuiona familia maana mwaka mzima nilikuwa na timu yangu ya Yanga hivyo ni muda wangu wa kwenda kupumzika," amesema.

6 COMMENTS:

  1. Usichelewe kuja kuliokoa jahazi

    ReplyDelete
  2. Ila Kuna penati mbili Congo walionewa aise

    ReplyDelete
  3. Kateni rufaa. Kila siku kulalamika tu.Ndio hulka ya migongo wazi.Kulalama tu.

    ReplyDelete
  4. Hivi mtu akisema "nakwenda kuiona familia" anakuwa amegoma?
    Uandishi wetu unafarakanisha kwamba mtu huyu ukienda kumhoji siku nyingine atakunyima ushirikiano.

    ReplyDelete
  5. Zahera bila viti maalumu hana chake katika ligi ya TZ hadi nje

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic