August 7, 2019


AZAM FC, mabingwa wa kombe la Shirikisho wametia timu nchini Ethiopia tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Fasil Kenema.

Mchezo wa kwanza Azam itaupiga Agosti 11 kabla ya kurudiana na timu hiyo baada ya wiki mbili ndani ya jiji la Dar.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa kikosi kipo salama na kila kitu kinakwenda sawa.

"Kikosi cha Azam FC kimewasili leo salama mjini Bahir Dar, Ethiopia na kufikia kwenye Hoteli ya Solyana na Jumapili tutacheza mchezo wetu wa kimataifa, tupo tayari kwa ushindani," amesema. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic