August 7, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kama Kocha Mkuu wa  Simba ataamua kuendelea kuvaa mavazi meupe hawezi kumshangaa kwani ni maamuzi yake.

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba anapenda kuvaa mavazi meupe akiamini kwamba yanabeba bahati ya ushindi hata jana pia uwanja wa Taifa alitupia mavazi hayo na timu yake ikashinda mabao 3-1 dhidi ya Power Dynamo.

Zahera amesema kuwa:- "Kwa upande wa mavazi kama yeye anapenda kuvaa mavazi meupe akiamini yana bahati hilo ni juu yake kwani kila mtu ana maamuzi yake.

"kwa sasa nami nina maamuzi yangu kama msimu uliopita nilikuwa nina mavazi yangu ambayo yalikuwa yananitofautisha na wengine, kama ilivyo upande wa magari ninaweza kutumia Mercedes Benz na asinipangie mtu," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Vipi lakini wiki ya wananchi imeishia wapi? Maandamano sijui mafuriko ya wananchi yameishia wapi? Kwa kiasi fulani Yanga day ilkuwa vurugu tupu.Na kama inavyosemekana Yanga wamepigwa pia kunako mapato. Kuna tofauti kubwa kati ya tamasha la Simba na Yanga. Simba wameonesha ukomavu na Yanga wana hitaji kujifunza.Timu ya simba ineonesha kiwango kizuri yaani Mashabiki wa Simba na wadau wake wote unaweza kusema gharama za muda na pesa zao kwenda kuiona timu yao zimelipa mia 100 kwa mia 100. Ila mahaba ni kitu cha ajabu sana kuna waandishi wa Yanga nadhani wanahoji uwezo wa Simba na wachezaji wao mmoja mmoja katika mechi simba walioshinda lakini wakati huo huo wanasifia uwezo wa wachezaji wa Yanga katika mechi mbovu ya sare tasa zidi ya kariobangi sharks ambao walichapwa na KMC kiulaini kabisa. Yanga wajitafakari na timu yao na waache kuendelea kusifia usajili wao kwani wakati wa vitendo umewadia kwa wachezaji wao kuonesha kile walicho nacho.

    ReplyDelete
  2. Waache mchekea nyani huvuna mabua.Kila mwenye macho anaona tofauti ya hizi timu. TIMU moja inapambwa na waandishi vipofu wenye mapenzi yasiyojenga. Fikiria kocha mzima anazungumzia sharti la kocha mwenzake halafu waandishi makanjanja wanacheka.Mwenzake Ibege kajiuzulu kwa matokeo mabaya ya AFCON.

    ReplyDelete
  3. Hawa waandishi huwashagilia watani kila wanapozishinda timu za mitaani Kwa magoli mengi bila ya kuwashauri kujipima na timu ngumu na kuilezea Ni timu ya kuitea moto Kwa nbali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic