INAELEZWA kuwa uongozi wa Biashara United kwa sasa umejipanga kuja na Tamasha maalumu litakalotambulika kwa jina la Biashara United Family likiwa na lengo la kuitambulisha klabu kwa wanachama.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Seleman Mataso amesema kuwa lengo kubwa la Tamasha hilo ni kutoa sapoti kwa mashabiki na kurejesha shukrani kwa mashabiki.
"Tamasha letu maalumu litapewa jina la Biashara Family ambalo linaanza Agosti 6 na litafika kilele Agosti 12 na lengo likiwa ni kuwatambulisha mashabiki timu yetu pamoja na wachezaji wetu.
"Tutafanya kazi ya kutambulisha wachezaji pia wiki moja tutafanya kazi maalumu kwa kuwatembelea yatima, wagonjwa na kuzindua matawi ya Biashara United na kilele chake tutacheza na Tusker FC kutoka Kenya," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment