KASSIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa kwa sasa ni ruksa kwa wawekezaji kuwekeza nguvu kubwa kwenye soka kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania.
Majaliwa alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Simba na Power Dynamo ambapo alisema kuwa anafurahishwa na maendeleo ambayo timu ya Simba imefikia hivyo ni fursa kwa timu nyingine kuiga mfano huo.
"Nimefurahishwa na uwekezaji wa Simba hasa ukizingatia kwamba kwa sasa mpira ni uwekezaji na unahitaji pesa nyingi, nimefurahi kuskia kwamba Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni (Harrison Mwakyembe) amekubali suala la uwekezaji hivyo ni fursa kwe wengine kuwekeza.
"Tunatambua uwepo wa muwekezaji ndani ya Simba ambaye ni Mo, tupo tayari kuona uwekezaji mkubwa unafanyika kwenye kila timu na kwa manufaa ya timu kwani lengo la Serikali ni kuona mafanikio," amesema.
Kabisa serikali hapo mmepaona na tunaamini kwamba sasa mmeamka katika Suala la michezo hasa mpira wa miguu.Kwani moja ya wizi uliobakia kwenye taasisi za umma ni huku kwenye football industry kwa baadhi ya watu kukataa uwekezaji kwa timu kama simba au Yanga kwa kujificha kwenye kichaka cha kuzilinda timu hizo kuendelea kuwa timu za wananchi lakini madhumuni yao ni kuendeleza ufisadi kunako timu hizo. Sekta ya michezo hasa mpira wa miguu ni sekta tajiri duniani hivi sasa na serikali inatakiwa kumka zaidi.Vile vile mpira wa miguu ni sekta mkombozi ya kupambana watoto wazuzuraji wasiokuwa na makazi maalum kutokana na matatizo ya wazazi. Mpira ni maliwazo au therapy kwa jamii katika kufarahia maisha baadala ya jamii kujikita kwenye matukio ya misiba peke yake iwe ya maisha magumu au matatizo ya kifamilia kwa hivyo serikali ipo haja ya kuekeza pia badala ya kuwaacha wawekezaji binafsi peke yake kuekeza.
ReplyDelete