KOCHA Mkuu
wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa kikosi kipo tayari kumaliza biashara
mbele ya Kagera Sugar mchezo wa ligi utakaochezwa uwanja wa Karume.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Said amesema kuwa wamejiandaa kutoa burudani kwa mashabiki
na kuleta ushindani wa kweli msimu mpya wa 2019/20.
“Tunatambua
mchezo utakuwa mgumu ila lazima tumalize biashara mapema, kikosi kitawakosa
wachezaji wawili ambao ni pamoja na Victor Hangaya na Joseph Kimwaga, wengine
wapo fiti, mashabiki wajitokeze,” amesema.
Meky Maxime,
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa hana mashaka na mchezo huo ana imani ya
kupata ushindi na kikosi chake wote wapo kamili gado.
Msimu
uliopita wa mwaka 2018/19 walipokutana uwanja wa Karume matokeo ilikuwa 0-0
hivyo leo kazi kubwa ni kutafuta rekodi mpya.
Azam FC: Waethiopia wanakuja
machinjioni watachinjwa
0 COMMENTS:
Post a Comment