KUELEKEA
kwenye mchezo wa ligi kuu leo kati ya Namungo FC dhidi ya Ndanda, uwanja wa
Majaliwa viongozi wa timu zote mbili wamesema kuwa lazima wafungue pazia kwa ushindi
ili kuwa na mwelekeo mzuri kwenye michezo inayofuata.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Hitimana Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesemawamefanya maandalizi ya kutosha kupata ushindi.
“Ni mchezo
wetu wa kwanza, tumefanya maandalizi ya kutosha kufungua pazia vema, hakuna
kinachotutisha kwani usajili wetu ni bora na wa viwango, mchezaji mmoja tu Dany
Gustavo tutamkosa wengine wapo vizuri,” amesema.
Kwa upande
wa Ndanda FC, kupitia Ofisa Habari wao Idrisa Bandari amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ushindani.
“Malale
Hamsini ndiye anayekinoa kwa sasa na amewapa mbinu nyingi wachezaji, mpaka sasa
hakuna majeruhi tuna imani utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji ushindi,”.
0 COMMENTS:
Post a Comment