August 13, 2019


DISMAS Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa klabu inaushukuru uongozi wa Azam FC kwa kuwapa gari wapinzani wao Township Rollers.

Kwenye mchezo wa Yanga na Township Rollers uliocezwa uwanja wa Taifa, wageni Rollers walitumia basi a Azam.

Ten amesema: "Azam FC walitupa basi kwa ajili ya kutusaidia sisi kama ilivyo utaratibu wa Caf kwamba mwenyeji anashughulikia ishu nzima ya mgeni nasi tuliongea na kampuni ya Azam ikafanya hivyo.

"Tunawashukuru sana kwa sapoti yao na kwa mchango wao, kila kitu kipo wazi na hivyo kusiwe na maneno kwamba Azam FC wametuhujumu," amesema Ten.

1 COMMENTS:

  1. Kwanini Balama Mapinduzi hayupo kambini Moshi? Haya maswali na wasiwasi wa mashabiki yanazidi kuvuma yaani pale ambapo mchezaji fulani anaanza kuwa tegemeo hapo ndipo mambo yanaanza kuzuka, mara majeruhi mara ana matatizo binafsi/kifamilia....ili mradi figisu figisu....wana Yanga sio wajinga wanajua kila Kinachoendelea kuna siku watatoka mafichoni na kuleta sintofahamu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic