August 13, 2019


KIKOSI cha JKT Tanzania kimejichimbia Visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimu vumbi Agosti 23.

JKT Tanzania mchezo wake wa kwanza itamenyana na Simba, Agosti 23 uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Abdalah Mohamed 'Bares' amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na hesabu ni kufanya vema.

"Kikosi kipo salama na wachezaji wana morali, hivyo kufanya vema ndio mpango wetu mkubwa kwenye ligi kuu Bara.

"Sapoti kwa mashabiki na wadau kwani tunaamini ligi itakuwa na ushindani mkubwa ila tupo tayari," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic