August 25, 2019



Na George Mganga

Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Muingereza, Dylan Kerr, amesema usajili wa kiungo Francis Kahata ambaye ni raia wa Kenya, utaisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Kerr amefunguka kwa kusema anamjua vema Kahata kuliko hata Simba wenyewe sababu amemfundisha kwa muda mrefu wakati akiinoa Gor Mahia FC ambayo Kahata alikuwa akiichezea.

Kerr ambaye yupo kwao England akiwa hana timu, anaamini uwepo wa Kahata utazidi kuifanya Simba iwe bora haswa anapocheza na Meddie Kagere ambaye naye alimfundisha wakati akiwa Gor Mahia.

"Usajili wa Kahata ni mzuri na utaboresha kikosi cha Simba kwani ni mzuri katika kumiliki mipira na hapotezi kirahisi, nimekuwa naye kwa muda mrefu na namfahamu.

"Uwepo wake utaifanya Simba izidi kuwa bora haswa kwenye idara ya kiungo, na akicheza na Kagere ambaye nilimfundisha nikiwa Gor Mahia, naamini kabisa timu itakuwa na makali.

"Sifa moja ya Kahata ni mtulivu na anaweza kutulia na mipira, anagawa pasi na zinafika kwa wenzake, kwakweli Simba wamelamba dume pale," amesema Kerr.

Kwa upande mwingine Kerr ambaye anafuatilia mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, amewashauri Simba kuhakikisha wanaongeza makali kwenye nafasi yao ya ulinzi ili kuzuia mabao kabla ya mechi na UD Songo ambayo wanacheza nayo leo jioni saa 10 kamili.

Ameeleza ili kuifanya timu iwe na rekodi nzuri ni vema ikahakikisha nyavu zake haziguswi, tofauti na msimu uliopita ilivyoruhusu mabao mengi haswa katika mechi za kimataifa za Ligi ya Mabingwa.

"Simba wanapaswa kutoruhusu mabao mengi langoni mwao, niliona msimu uliopita walikuwa na tatizo kubwa kwenye ulinzi, hilo vema wakalizingatia," alisema.

1 COMMENTS:

  1. Umenena Kerr. Haina maana kushangilia goli huku ukijua uwezekano wa wapinzani kurudisha ni mkubwa kwasababu ya makosa ya kujirudia rudia katika sehemu sehemu ya ulinzi na vingi wakabaji. Washabiki wa Simba hawajawahi kuiacha timu yao katika mazingira yeyote yale. Timu ipate mafanikio au la. Hawahitaji kuhimizwa kuishabikia timu yao hayo ni mapenzi yao na wala sio majukumu yao. Mwekezaji, Bodi nzima, Rais wa klabu, menejimenti, watumishi wote na benchi la makocha na wachezaji watimize wajibu wao. Simba ni klabu kubwa Afrika. Ni muda sasa wa kufikia mafaniko makubwa zaidi. Nguvu ya mashabiki uwanjani ni baada ya timu nzima kuonesha uwezo wa kuwa ni timu kubwa kwa kuonesha kiwango katika kila idara. Isitumike nguvu ya mashabiki uwanjani kuficha udhaifu wa timu yenyewe. Tutaaibika tena huko mbele tuendako. Nguvu Moja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic