August 25, 2019


Dalili zinaonesha Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ataendelea kusalia kunako timu hiyo baada ya ushindi wa jana dhidi ya Township Rollers.

Yanga ilifanikiwa kuitandika Rollers bao 1-0 ikiwa ugenini kupitia kwa Juma Balinya mnamo dakika ya 42 kwa njia ya fauli kipindi cha kwanza.

Uhsindi huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unakuwa unampunguzia presha Zahera ambaye awali ilikuwa ikielezwa anaweza akaondoshwa Yanga endapo angefungwa mechi hiyo.

Taarifa zilielezwa kuwa kulikuwa na mgongano wa chini kwa chini baina ya Zahera na uongozi haswa kuchelewa kuripoti kambini baada ya kambi ya AFCON akiwa na timu ya taifa ya Congo kumalizika.

Kuchelewa kwake kulizua maswali mengi ambayo yaliifanya Yanga ikae muda mrefu kambini kujiandaa na msimu mpya bila uwepo wake lakini baadaye alirejea.

3 COMMENTS:

  1. Ninyi waandishi no wachonganishi sana na ndo munaharibu Mpira was bongo kqa kuandika vitu vya uongo sana

    ReplyDelete
  2. Tumwache kocha afanye kazi yake isitoshe ndo kwanza anapanga first 11

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic