BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, 'Tanzanite' amesema kuwa wachezaji wake wanapaswa pongezi kwa kupambana.
Tanzanite imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo miwili ya michuano ya COSAFA kwa kuanza mbele ya Botswasana ushindi wa mabao 2-0 na jana mbele ya Eswatini mabao 8-0.
"Wachezaji wanastahili pogezi kwani wamepambana mwanzo mwisho bila kukata tamaa, awali walikuwa na hofu pamoja na kutozoea mazingira kwa haraka.
"Kuwahi kwetu kufika Afrika Kusini kumetujenga na kutufanya tuwe vizuri, mashabiki waendelee kutupa sapoti mwanzo mwisho," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment