August 7, 2019


BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake 'Tanzanite' amesema kuwa akili za timu pamoja na wachezaji ni kwenye mchezo wao wa nusu fainali dhidi timu ya Afrika Kusini.

Tanzanite imealikwa kwenye michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini na imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo miwili kwa kuanza ule wa Botswana kwa ushindi wa mabao 2-0 kisha Eswatini mabao 8-0 kabla ya jana kupoteza mbele ya Zambia kwa kufungwa mabao 2-1.

"Mchezo wetu mgumu utakuwa mbele ya Afrika Kusini ambao unakuja na tunajua utakuwa mgumu kama ambavyo ulikuwa mchezo wetu dhidi ya Zambia.

"Tumejipanga na tunapambana kupeperusha Bendera ya Taifa nafasi ipo na kila kitu kinawezekana," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic