August 7, 2019


UONGOZI wa KMC umesema kuwa kwa sasa maandalizi yanaendelea kwa kasi kuelekea kwenye mchezo wao wa kimataifa dhidi ya AS Kigali utakaochezwa nchini Rwanda.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa kwa sasa maandalizi yamepamba moto na hesabu zao ni kuleta ushindani kwenye michezo ya kimataifa.

"Tunatambua kwamba tuna kazi ya kupeperusha Bendera ya Taifa hivyo tunafanya kweli mwanzo mwisho tukiwa ugenini kwani hizo ni hesabu zetu na mipango ya mwalimu.

"Tuna uzoefu na mazingira ya Rwanda hivyo hatuna mashaka na kile ambacho tunakwenda kukifanya hivyo ni wakati wa mashabiki kutupa sapoti ili tufanye vema," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic