UONGOZI wa Yanga umeamua kutupa dongo kimtindo kwa wapinzani wao Simba kuhusu ubora wa jezi zao.
Kwa sasa vita kubwa iliyopo ni nani ana jezi bora huku kila timu kati ya Simba na Yanga zikivutia kamba kwao kuonyesha kwamba ubora wao ni wa hali ya juu.
Dismas Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa wapinzani wao wanatambua kuwa Yanga wana jezi bora na wanapenda kuzinunua ila wamekuwa wakizikosa madukani.
" Wapinzani wetu wanajua kwamba tuna jezi nzuri na wao wanapenda kuzivaa ila wanazikosa hivyo kwa sasa tumejipanga kuona kwamba zinapatikana kila kona.
"Kwa sasa ni suala la mashabiki wetu wa Yanga kutafuta jezi halisi kwenye maduka yetu ya GSM huko watapata jezi nzuri mfano wake hakuna," amesema.
Haya sio maonesho ya staili ya mavazi na Nani kapendeza lakini ni mashindano ya kutandaza soka. Hawasifiwi akina Kakolanya, Ajibu na na Michael Kwa kupendeza walichovaa lakini jinsi uhodari WA kupachika magoli na kuzuwia magoli kuingia
ReplyDeleteKaka unknown umepiga msumari wa moto!! Hongera sana
DeleteKwahakika maneno muwafaka yakweli tupu bila ya kubisha na hilo ndio dongo la kweli
ReplyDeleteKMC kumbe hatari Ni ushahidi wazi wamepinduwa gogo lililowashinda tembo. Hahaha. Tutaona mambo mwaka huu
ReplyDeleteMikia mtapata tabu Sana mwaka hu
ReplyDeleteAnaependa rangi ya kijivu hawezi hata kidogo kuisifu chanikiwiti kuwa ni nzuri. Tuache mashindano ya kitoto tucheze mpira
ReplyDelete