HARRY Maguire, anaingia kwenye rekodi ya mabeki ghali duniani baada ya usajili wake kukamilika na Manchester United kuthibitisha kuwa wametumia pauni milioni 80 likiwa ni dau la usajili wake kutoka Leicester City.
Maguire amesema: "Nimefurahi kumwaga saini kwenye klabu kubwa kama hii, nina furaha kubwa kuwa hapa.
"Shukrani nyingi kwa mashabiki na viongozi wa Leicester City pamoja na kila mmoja ndani ya timu kwa sapoti yao kubwa kwa muda ambao nilikuwa nao.
"Kama Manchester United wanagonga mlango kwako hiyo ni dili kubwa na bahati pia hivyo kwangu ilikuwa nafasi adimu.
"Nimeongea na Meneja, Ole Gunnar Solskjaer nimeona kuna kitu anakitengeneza hivyo nina imani tutakuwa na kikosi imara msimu utakapoanza," amesema.
Nyota huyo amesaini kandarasi ya miaka sita ndani ya United amevunja rekodi ya beki Virgil Van Dijk aliyopewa mwaka 2018 wakati anajiunga Liverpool ya pauni 75.
0 COMMENTS:
Post a Comment