August 5, 2019



Uongozi wa Yanga umeishtaki Kampuni ya Selcom Tanzania, serikalini kutokana na utendaji wao wa kazi mbaya ambao ulikuwa wa wizi na rushwa uliotokea kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.


Kilele hicho cha Wiki ya Mwananchi kilikuwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa timu hiyo kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Kariobang Shark’s ya Kenya na Yanga kwa timu hiszo kutoka sare ya bao 1-1.



Akizungumza na Waandishi wa Habari, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa hawakuridhishwa na utendaji kazi wa Selcom ambao kama ukiendelea, basi serikali utapoteza mapato mengi.


Mwakalebela alisema kuwa mawakala wa kampuni hiyo ndiyo walikuwa tatizo waliokuwa wanauza tiketi mara mbili kwa mashabiki waliokuwa wamejitokeza.


“Leo Jumatatu tunatarajia kuandika barua kwenda serikalini kwa ajili ya kuwataarifu wizi na rushwa iliyokuwa inafanyika katika kilele chetu cha Wiki ya Mwananchi.


“Kikubwa tunataka kuwafahamisha tatizo hilo lililotokea siku hiyo ya tukio na mbaya zaidi siku hiyo tiketi za Simba Day zilizopangwa kutumika kesho zimetumika kwenye tamasha letu, hivyo tunashinda kufahamu hizo pesa zinakwenda Simba au Selcom,” alihoji Mwakalebela.

6 COMMENTS:

  1. Hii timu imekuwa timu ya kulalamika kila kukicha.Wameshika hizo tiketi za Simba Day?Mashabiki wao walikubalije kuuziwa tiketi mara mbili wakijua wanaihujumu timu yao kama madai haya ni kweli?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuhusu tiketi za simba day siwezi ongea chochote ila jana hats mjmi yamenikuta kwani niliuziwa tiketi na wakala wa selcom kuingia ktk mageti ikagoma masna inaonekana ilishatumika...tayari club imeshapigwa mbaya zaidi wale wakagua tiketi wanakwamboa subiri utapita na mwenye tiketi yaani ji aibu jamani

      Delete
  2. IGA UFE
    Tanzania's Simba on the road to change
    https://www.bbc.com/sport/football/49220480

    ReplyDelete
  3. Ilichukua hatua gani?Kama uliona madudu yanafanyika utanyamaza basi na wewe ni guilty through being silent when a crime is committed.

    ReplyDelete
  4. Yanga huu mwanzo wa kulalamika mpakaligi nzima mtakuwa mnalalamika tu kama kawaida yenu.Bado zahera zamu yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic