KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga, Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amekiona cha moto baada ya ‘wahuni’ kufanya utapeli kwa kutumia akaunti yake.
Mnyarwanda huyo ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao, wengine baadhi ni Patrick Sibomana, Maybin Kalengo, Farouk Shikalo na Sadney Urikhob.
Sibomana amesema kuwa watu wasiojulikana wametengeneza akaunti ‘fake’ ya Instagram wanaoitumia vibaya kuwatapeli baadhi ya mashabiki wa Yanga baada ya kusajiliwa na kutangazwa mchezaji wa Yanga amewatahadharisha mashabiki wa Yanga kuwa makini na matapeli hao wanaotaka kujipatia fedha kwa kutumia jina lake.
“Labda niwatajie akaunti yangu ninayoitumia kwenye akaunti zangu za Instagram na Facebook kuwa natumia Issa Walcott na siyo Issa Bigirimana, ni vema wakalifahamu hilo katika kuepuka kutapeliwa na vibaka.
“Zipo akaunti nne ‘fake’ zilizotengenezwa na wezi hao ambazo siyo zangu, wanazitengeneza kwa nia mbaya ya kutaka kuwaibia mashabiki wa Yanga kwa kuwaomba fedha.
“Niwaombe hao wezi kuachana na hizo akaunti, sitaki kuona hili likiendelea la wizi wa fedha na mashabiki wa Yanga hiyo nyingine ndiyo akaunti yangu,” amesema
0 COMMENTS:
Post a Comment