August 5, 2019


MOHAMED Dewji, 'Mo' Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba amesema kuwa uwekezaji wake wa bilioni 20 haupo kwenye mpango wa Uwanja wa Bunju.

Simba leo imeweka jiwe la msingi kwenye viwanja vyake viwili vya Bunju ambapo Mo amesema kuwa haipo kwenye mpango wa kuwekeza.


 "Uwanja huu unajengwa kwa bajeti inayojitegemea tofauti na ile sh.bilioni 20 ambazo nilisema nitawekeza, ninachotaka tuwe na miundombinu mizuri na tunajenga viwanja viwili ambapo kimoja ni cha nyasi bandia na kingine ni cha nyasi asilia," amesema. 

Uwekaji wa jiwe la msingi leo ulihudhuriwa na mashabiki wa Simba pamoja na viongozi ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Dr. Harrison Mwakyembe.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic