OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kesho lazima aje na mtindo mpya wa utambulisho baada ya ile ya awali kudai wameiba watani zake jana.
Jana Yanga walihitimisha kwa kishindo siku ya Mwananchi uwanja wa Taifa ambapo walicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Kariobangi Sharks ya Kenya pamoja na kuwatambulisha wachezaji wapya, kesho ni zamu ya Simba ambapo wao watacheza na Power Dynamo.
Kwenye siku hiyo ambayo itahitimisha SportPesa Simba wiki wamepanga kutambulisha wachezaji na jezi mpya watakazotumia msimu ujao.
Kupitia Ukurasa wa Instagram, Manara ameandika namna hii:"Yupo Haji Manara mmoja tu bongo.Uhai na Majaliwa tu ila kesho taifa hili tutalisimamisha kupisha Simba Day.
Wameiga style yangu ya utambulisho ila kesho nakuja vingine. Hapa ni University kamili ,hadi PhD natoa.
Ukikosa kesho umeliwa," amesema.
MANARA BOYA TU, ACHANA NA CC
ReplyDeleteHAJCKII AIBU KAKA ETU ANATAKA UMAARUFU KUPTIA YANGA MPK KCHEFCHEF
ReplyDeleteChura zimewashuka.Husda na fitina hazisaidii.Haji Manara ndio kiboko yenu.Mkilala mnamuota.
ReplyDeleteHivi mnafaham kazi ya msemaj wa team....hapo yupo kwenye eneo lake mwachen ajigambe
ReplyDelete