KIKOSI cha KMC kesho kinatarajia kukwea pipa kielekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Kigali.
KMC itacheza mchezo wake wa kwanza Agosti 10 nhini Rwanda na AS Kigali kabla ya kurudiana na wapinzani hao jijini Dar baada ya wiki mbili.
Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa:-" Wachezaji 18,benchi la Ufundi pamoja na viongozi watakua katika msafara huo,wachezaji wetu wa kigeni wanne watakosekana kwa kukosa leseni kutoka CAF.
"Besala Bokungu, Melly Sivirwa, Jonathan Nahimana pamoja na Mugiraneza jean Baptiste na sababu kubwa ni kuchelewa kwa kusajiliwa kwao na watatumika katika raundi ya pili ya mashindano haya baada ya kufanikiwa kuitoa As Kigali,". amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment