NYOTA watatu wa kikosi cha KMC leo waabaki Bongo huku wengine 18 wakikwea pipa kuelekea nchini Rwanda.
KMC inaifuata AS Kigali ya Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Kigali mchezo utakaochezwa Agosti 10.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa wachezaji hao watatu watabaki kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
"Cliff Buyoya, Charles Ilanfia na Ramadhan Kapela hawa watakosekana kutokana na kupata majeruhi ila wameanza mazoezi mepesi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment