JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa kazi kubwa iliyopo kwa sasa kwa kikosi cha Simba ni kupambana kupata matokeo kwenye mchezo wao wa kimataifa.
Simba kesho inakwea pipa kuelekea Msumbiji kwa ajili ya kucheza mchezo wa awali na UD Songo mabingwa wa Msumbiji utakaopigwa Agosti 10 nchini Msumbiji.
Bocco amesema,:"Tuna kazi kubwa kimataifa na kila mchezaji anajua jukumu lake jipya na namna ambavyo anapaswa kufanya.
"Mashabiki wanapenda kuona timu inapata matokeo nasi tunakwenda kupambana kwa ajili ya Taifa hivyo sapoti yao ni muhimu kwetu," amesema.
Simba itakwea ndege binafsi ili kuepuka usumbufu wa kupanda ndege mbili itarejea baada ya kumaliza mchezo huo ili kujiandaa na mchezo wa ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.
Mungu itabariki timu zote za Tanzania,mwaka huu wetu.ameena
ReplyDeleteAmina
ReplyDeleteUkiona mtego umemnasa kanga husemi Asante kanga lakini unasema Asante mtego na kuhusu asasi hii kubwa iliyojikusanyia mapenzi na heshima hstusemi Asante asasi lakini tunasema Asante kiongozi Moo Kwa hekima na ukarimu wake usio na mpaka Kwa asasi hii pamoja na timu na idara yake yenye kila Aina ya busara na kuuweka mkono wake wazi na mapenzi yake Kwa star wote kama mzazi na watoto wake ambapo hatukuwahi kusikia hata mara moja malalamiko au kitu kinachoitwa mgomo. Huyu Ni Moo WA watu. Simba ni timu maridadi inangara na inapendeza raha kuitazama
ReplyDeleteSimba tunajua ni timu makini ila wanatakiwa kuwa na tahadhari kubwa Msumbiji.Udhaifu wa Simba kutokujiamini wanapokuwa ugenini ambao uliwaathiri sana mwaka jana tunaimani utakuwa umefanyiwa kazi. Kinachowaponza Simba ni wachezaji wake kukosa kujiamini wanapokuwa ugenini na kama watalifanyia kazi hilo basi watafanikiwa msimu huu.Tatizo jengine Simba wamekuwa wakicheza mechi za ugenini bila ya kanuni inayosema hutakiwi kumuogopa mwenyeji wako lakini unatakiwa kumuheshimu.Simba msimu uliopita klabu bingwa Africa walishindwa kabisa kuzicheza mechi za ugenini sababu kubwa ni kukosa umakini katika dakika za mwanzoni mwa mchezo na hata walipokuja kuamka ilikuwa too late.
ReplyDeleteTunaamini hata aina ya wachezaji binafsi waliopo wanauzoefu na mashindano ya kimataifa na pia wamecheza mechi nyingi za kimashindano, tofauti na idadi kubwa ya wachezaji wa msimu uliopita ambao wengi walikuwa wageni katika mashindano makubwa hali ambayo iliwaongezea uoga ugenini na hata nyumbani. Makosa mengine ya msimu uliopita imani yetu ni kuwa yatakuwa yamefanyiwa marekebisho, ingawa kosa la kuchelewa kujipanga kwa wachezaji wakati wa kupigwa mipira ya adhabu kuelekea langoni kwetu, limekuwa bado lipo, hilo limeonekana hata katika goli ambalo walipata Power Dinamor. Lifanyiwe kazi zaidi.
ReplyDelete