SELEMAN
Matola, Kocha wa Polisi Tanzania amesema kuwa kikosi chake kipya kinatengamaa na
kitaleta ushindani kwenye ligi msimu ujao.
Polisi
Tanzania imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu na itakuwa miongoni mwa timu 20
ambazo zitashiriki ligi inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa maandalizi ya mwisho kwa sasa yapo
sawa wana imani ya kufanya makubwa ligi ikianza.
“Tupo sawa
na kikosi chetu kina moto wa kutosha kabla ya ligi kuanza hivyo imani yetu ni
kufanya makubwa msimu utakapoanza hasa ukizingatia ni kikosi kipya lazima
wachezaji wawe na mambo mapya.
“ Kwenye
ligi hatuna hofu iwe ni Simba, Yanga,
Azam tutapambana, kikubwa ni sapoti na kushirkiana," amesema.








0 COMMENTS:
Post a Comment