UONGOZI wa Paris Saint Germain (PSG) inaaminika kuwa upo tayari kumuuza nyota wao raia wa Brazil, Neymar Jr lakini sio kwa kuwauzia Barcelona.
Neymar aliwaambia PSG kuwa katika kipindi cha usajili hayupo tayari kubaki ndani ya klabu hiyo anataka kurejea Barcelona.
Katika kuashiria kuwa PSG wanataka kumkomoa Neymar nao pia inaaminika kuwa haina mpango wa kumuachia kwenda Barcelona kwa kuwa hawataki kufanya biashara nao.
PSG na Barcelona hazina uhusiano mzuri ambapo tofauti baina yao zilizababishwa na nyota huyo mwaka 2017 wakati huo Barca iligoma kumuuza nyota huyo.
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi inasemekana amekuwa na msimamo mkali wa kutozungumza na Barcelona kuhusu dili la Neymar.
0 COMMENTS:
Post a Comment