PAUL Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa yeye ni kwa haua ambayo Yanga wameanza kwa sasa ni hatua kubwa na inahitaji pongezi.
Yanga jana walihitimisha siku ya Mwananchi kwa kucheza mchezo wa kirafiki na Kariobangi Sharki uwanja wa Taifa na walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Makonda amesema"Naona Yanga wameanza vizuri na wamerejea kwenye ubora wao nimeongea na viongozi na nimewapongeza kwa jambo ambalo wamelifanya.
"Mimi ni mpenzi wa Yanga, shabiki wa Azam, mkereketwa wa KMC lakini mwanachama wa Simba.
"Tunaamini wameanza vizuri lakini timu hizi kubwa ambazo ni Yanga, Simba, Azam na KMC zikifanya vizuri imani yetu mpira wetu utakwenda mbali sana," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment