August 13, 2019


Daktari wa timu ya Yanga Edward Bavu ameivuka na kusema kuwa beki wa timu yao Paul Godfrey 'Boxer' atakosekana dimbani kwa wiki kadhaa.

Boxer atakuwa nje kutokana na kupatwa na majeraha katika mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Bostwana.

Kutokana na kuumia kwake, Bavu amezungumza kuwa Boxer ataukosa tena mchezo wa marejeano dhidi ya Rollers utakaopigwa huko Gaborone, Botswana.

Yanga tayari imeshaanza kambi ambapo leo imeondoka jijini Dar es Salaam kuelekea kaskazini mwa Tanzania kujifua kabla ya safari ya kuelekea Botswana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic