August 8, 2019


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hakuna rekodi ambayo imewahi kuvunjwa na timu yoyote ya kujaza uwanja wa Taifa mapema tangu walipofanya wao Julai 28 mwaka 2016 kwenye michuano ya kimataifa ambapo Yanga ilicheza na TP Mazembe.

Yanga imesema kuwa kwenye mchezo huo mapema saa 6 mchana walikuwa wamejaza uwanja huo na mageti yote kufungwa ili kuzuia mashabiki waliokuwa nje wasiingie ndani.

Barabara zote zilijaa wananchi na ilibidi zifungwe na Polisi walitumika kuzuia wananchi wasiingie ndani ya uwanja na kuwatuliza wale waliokuwa nje.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kwa sasa mashabiki wanatakiwa wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa siku ya jumamosi kushuhudia ushindani kati yao na wapinzani wao Township Rollers uwanja wa Taifa.

8 COMMENTS:

  1. Vipi muandishi mnasema hivo. Kwani hamkuona takwimu ya Yanga na mapato yake na Ile ya mahufhurio ya Simba na mapato yake. Mahufhurio Ya Simba na mapato yake yalikuwa makubwa Sana kuliko ya Yanga au ndio hukuona na Huna habari nayo

    ReplyDelete
  2. Uwanja kujaa inaendana na mapato klabu inayopata kutokana na tiketi.haikuwa hivyo msimu uliopita kwa Yanga

    kweli kabisa wakija AS Vita kucheza na Simba uwanja unajaa ili kushangilia wakongo...Ija Biashara dar kucheza na Yanga uwanja mtupu...Wajaze basi uwanja hata wakiwa wanachenza na timu za bongo inaongeza mapato ..

    ReplyDelete
  3. MIKIA INACHEKESHA KWELI DUNIANI HAPA.

    ReplyDelete
  4. Walizania Ni wao ndio waliopata mahudurio na mapato makubwa zaidi

    ReplyDelete
  5. Eti mechi watu walioingia bure ndio anajivunia naye.Kulikuwa hamna kiingilio waliingia wapende mpira wote.Kweli huyu Dismas hamnazo .

    ReplyDelete
  6. Hata kimapato Simba ndio iliongoza katika timu zote msimu uliopita.

    ReplyDelete
  7. Huo mwaka unaosema mlifanya kuzoazoa mashabiki. Baada ya kuona mashabiki tia maji manji alijitoa mhanga kuwalipia watu wote nakumbuka washabiki wliingi bure.

    ReplyDelete
  8. Tunajua match anayoisema.TP MAZEMBE VS YANGA 2016-ilikua BURE,Manji alitangaza BURE ndio maana watu walijaa mapema

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic