August 24, 2019


Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Taifa wa Bostwana kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Township Rollers katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imepata ushindi mnamo dakika ya 42 kupitia kwa Juma Balinya aliyefunga kwa mkwaju wa faulo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam, Yanga iliweza kwenda sare ya bao 1-1.

Kipa wa Yanga Metacha Mnata aliweza kudaka penati ya Rollers kipindi cha pili na kuweza kuipunguzia kazi ya kuanza kusaka bao jingine.

Ukiachana na Yanga, Azam FC pia ilikuwa na mchezo leo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo imefanikiwa kuichakaza vibaya Fasil Kenema kwa mabao 3-1 ambapo katika mechi ya kwanza walifungwa 1-0.

12 COMMENTS:

  1. Benchi la ufundi na uongozi mzima sasa uanze maandalizi mapema kwa mechi ngumu dhidi ya ZESCO United na sio kwenda kuweka tena kambi Moshi na kucheza na timu zisizo na ushindani.

    ReplyDelete
  2. wewe shabk wa simba kama ungekuwa wa yanga kitu cha kwanza ni kuwapongeza jadili yako. hongeren yanga mana muliambiwa hamushidi ugenini kwa ujumla tmu za tanzania zibadilike tusiwe na dhana ya nyumban hatok mtu kuanzia sasa yanga wameweka hctoria ya kushnda popote.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inaonesha kichwani mwako kumejaa makamasi na sio ubongo.Mtoa maoni hapo juu katoa maoni mazuri tu kuhusiana na maandalizi ya nguvu kwa ajili ya mchezo unaokuja wewe kwa umbulula wako unaleta hoja ya kupongeza!!!!amesisitiza kuhusu maandalizi ya nguvu suala ambalo hata kocha Zahera aliizungumzia kabla timu haijaenda Botswana.Pongezi zilishatolewa baada tu ya mchezo na kujipongeza kwa sana kwa kuvuka hatua moja

      Delete
    2. Waliwatoa mwaka 2017 rollers na nyie mmewatoa hakuna Cha kujisifia ambacho ni suprize mmefanya,mmeshinda kwa Gori la free kick si la move Koo tuliza mkia wenu vyura

      Delete
    3. We ulitaka washinde kwa goli gani? Kwani walifikaje kwenye goli la wapinzani na kupata hiyo free Kick? Inawezekana huyu hajuwah hata kucheza mpira wa makaratasi kabisaa. Maana hana hoja hata mtu aliyecheza timu ya darasa akiwa shule ya msingi anakuzidi uelewa wa magoli. Mbona hujazungumzia ile penalty waliyopewa wapinzani wa Yanga na kuishia mikononi mwa golikipa? Unapokuja hapa kuzungumza kwenye forum kama hii unapaswa kuwa na hoja badala ya ushabiki usio na kichwa wala miguu ambao hata mtu asiye na macho anakuona unakosea

      Delete
  3. Hongera Yanga Africa, timu inastahili kupongezwa kwa ushindi hasa wa ugenini, pamoja na pongezi benchi la.ufundi lifanyie kazi idara ya kiungo bado inashimdwa kutengeneza nafasi za magoli kwa watumiaji, mechi na Zesco ni ngumu na tusije kosea tena na kushindwa kumaliza mechi hapa nyumbani maana huu umekuwa ugonjwa wetu Yanga miaka mingi sasa team inakuwa na confidence inapokuwa nje ya nchi. Maandalizi yaanze haraka na wanachama pamoja na mashabiki na wapenzi tuipe support timu yetu pendwa kwa kwenda mpirani na kujaza uwanja

    ReplyDelete
  4. Kabisa mdau wa kwanza hapo juu hakuna muda wa kupoteza kibarua kigumu, maandalizi mapema, sasa ni Zesco na Lwandamina, coach anatujua vizuri na mpira wa Zambia uko juu.

    ReplyDelete
  5. Kwa hy kosa lake kuipokea timu yake kusonga mbele?

    ReplyDelete
  6. hao wanaopost mambo ya ajabu n simba wanafk tu leo wanajfanya kutoa ushaur

    ReplyDelete
  7. na kla tmu tutayocheza nayo watasema ngumu yanga tmu kubwa na hlo wamezhrsha jana ugenini wengne kushnda mpk nyumban udhaifu tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic