JUMAPILI ya wiki hii, wawakilishi wa Taifa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam FC wanatarajia kukwea pipa kuwafata wapinzani wao Triangle, nchini Zimbabwe.
Azam FC ina kazi ya kutafuta ushindi kwenye mchezo wa marudio baada ya kupoteza mchezo wa kwanza mbele ya Trangle United kwa kufungwa bao 1-0 wakiwa nyumbani.
Msafara wa Azam FC utaondoka kwa mafungu matatu lile la kwanza likiwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo litaongozwa na Kocha Msaidizi, Idd Nassor Cheche.
Kundi la pili la msafara huo, litaondoka Septemba 23 na wachezaji watano waliokuwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wanaojiandaa na mchezo dhidi ya Sudan, wakiwa sambamba na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, ambaye ni Kocha Mkuu wa muda wa Stars.
Msafara wa mwisho utakuwa na viongozi wakuu wa timu hiyo, watakaoungana na timu hiyo siku chache za mwisho jijini Bulawayo utakapopigwa mchezo huo Septemba 28 mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment