September 18, 2019

ADAM Salamba, mshambuliaji wa timu ya Simba ambaye amejiunga kwa mkopo na timu ya Al Jahra SC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Taiwan barani Asia kwa sasa anaogelea midola baada ya kusaini kandarasi ya miaka mitano yenye mkwanja mnono.

Salamba amesema kuwa kwake ni sehemu ya mafaniko kutimiza ndoto zake za kucheza nje ya nchi na atapambana kuipeperusha bendera ya Taifa.

“Nimesaini kandarasi ya miaka mitano huku Al Jahra ninaamini ni sehemu ya ndoto yangu ambayo nimeiota kwa muda mrefu, shukrani kwa viongozi wangu wa Simba, mashabiki pamoja na Serikali kwa sapoti yao licha ya kushindwa kuitumikia kwa muda klabu ya Namungo,” amesema.

Kwenye mkataba wa Salamba wa sasa huko Asia atapewa gari maalumu la kwendea mazoezini pamoja na la kutembelea pia atapewa nyumba yenye wafanyakazi huku mshahara wake ukiwa ni dola 4000 kwa mwaka na kila mwaka ataongezewa dola elfu moja.

Timu hiyo ya Salamba imeshiriki mara 21 kwenye Ligi Kuu nchini humo na ina taji moja la ligi ililolitwaa mwaka 1990 na inatumia uwanja wake Mubarak Al-Aiar.

5 COMMENTS:

  1. Tazama lugha aliyoitumia. Huyu mtoto Ni muungwana na hakusahau ihisani na hana hasada na hayo ndio yatayompaisha kwasababu Mungu anakuhisabu Kwa nia yako

    ReplyDelete
  2. Dola 4000 kwa mwaka!huu ni utani,jaribuni kuwa makini kidogo hata kama hamkwenda shule,halafu mnaandika eti kuogelea minoti

    ReplyDelete
    Replies
    1. mi pia nashangaa 4000 kwa mwaka pathetic!!! pro???? sio vitu vya kuweka heading za namna hiyo pls

      Delete
  3. Hivi huwa Waandishi wa Platform hii huwa mna haraka ya namna gani ku post habari ikiwa na makosa mengi namna hii?

    Kwanza Salamba kaenda KUWAIT sio Taiwan.
    Pili Mshahara wa $ 4,000 ni kwa mwezi sio kwa Mwaka.

    Pia kuna Vitu mnapaswa kuviweka wazi, mfano taarifa ya MANKA EDWARD aliyekuwa na Mkataba na Yanga, imesemwa wazi kuwa Yanga hawajamuuza, Walitoa barua ya kumwachia kwa Makubaliano ya kupata 20% iwapo Manka atauzwa toka Club yake mpya.

    Sasa tukija kwa Salamba how come ametolewa kwa Mkopo toka Simba then a sign contract ya miaka 5?

    Mchezaji gani anayeenda kwa mkopo kwenye team mpya hafu aka sign new deal?

    Waambieni wasomaji wenu ukweli ama Muwe mnauliza kutoka kwenye Source.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic