UONGOZI wa
Azam FC umesema kuwa kwa sasa hauna cha kuhofia mbele ya wapinzani wao Triangel
United kwa kuwa wamejifunza kupitia makosa na leo watapindua meza kibabe.
Azam FC
ilikubali kuchapwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho
uliochezwa uwanja wa Azam Complex hivyo leo wana kibarua cha kufunga mabao
zaidi ya mawili.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam Fc Jaffary Maganga amesema kuwa
mipango ipo kamili na wana sapoti kubwa ya mashabiki wa Zimbabwe.
“Tupo vizuri
na tuna amini tutapata matokeo chanya kwenye mchezo wetu wa pili ukizingatia
kwamba kuna mashabiki wa Azam FC ambao wapo huku Zimbabwe wameahidi kutupa
sapoti.
“Mipango ya
Kocha ipo sawa ni suala la muda tu kupindua meza, mashabiki waendelee kutuombea
dua ili tufanye vema na turejee na ushindi Bongo,” amesema Maganga.







0 COMMENTS:
Post a Comment