September 15, 2019



MCHEZO wa kwanza hatua ya Kwanza kwenye Kombe la Shirikisho kwa kikosi cha Azam FC dhidi ya Triangle United umeongezeka uzito kwa wawakilishi wa Tanzania baada ya kupoteza mchezo.

Bao pekee la wapinzani wa Azam FC, Triangel United ya Zimbabwe lilifungwa dakika ya 34 na Ralph Kawondera kutokana na uzembe wa safu ya ulinzi wa Azam FC.

Licha ya Azam FC kupewa sapoti kubwa na mashabiki waliojitokeza uwanja wa Azam Complex hayakuzaa matunda kwani safu ya ulinzi ya Triangle United ilikuwa ngumu na ikajilinda na hatari zote.

Sasa Azam FC ina kazi nzito ya kwenda kutafuta matokeo ugenini kwenye mchezo wa marudiano unaoatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 27-29 nchini Zimbabwe.


Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza wa kimataifa  kwa Azam FC kupoteza kwa mara ya kwanza uwanja wa nyumbani kati ya tisa ambayo walishaicheza tangu mwaka 2008. 

Mzigo wa Azam Fc kwa sasa ni kuongeza spidi ya kutafuta mabao zaidi ya mawili kwenye mchezo wa marudio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic