KOCHA Msaidizi wa timu ya Biashara United ya Mara, Omari Madenge amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kubeba pointi tatu mbele ya Simba mchezo wa ligi kuu utakaochezwa leo uwanja wa Karume.
Biashara United inaelezwa kuwa imeachana na Kocha Mkuu Amri Said kutokana na kuwa na matokeo mabovu kwenye mechi za mwazo za ligi kwani katika michezo minne waliyocheza mpaka sasa wametoa sare moja na kupoteza michezo mitatu.
Madenge amesema kuwa hesabu kubwa ni kupata poiti tatu muhimu kwani maandalizi yapo sawa na kila mchezaji ana morali kubwa kupata matokeo mbele ya Simba.
"Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila hilo halitupi mashaka kwani kila kitu kinakwenda sawa na maandalizi yetu yapo vizuri ni suala la muda tu kuamua.
"Kuhusu alipo Kocha Mkuu hilo bado sijajua ila alichoniambia yeye ni kwamba ana homa na nimeachiwa timu kwa muda habari nyingine juu yake sina," amesema.
Biashara mpaka sasa ina pointi moja pekee katika mechi nne ilizocheza ikikamata nafasi ya 18 Mwenyekiti Wa timu hiyo Selemani Mataso amesema kuwa mustakabali wa Kocha utatolewa baada ya siku mbili.
0 COMMENTS:
Post a Comment