September 29, 2019


SELEMAN Matola, Kocha wa Polisi Tanzania amesema kuwa wachezaji wake walipambana kutafuta pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting walikwama kwa kukosa bahati.

Polisi Tanzania jana ilipoteza mchezo wake wa kwanza ndani ya ligi kwa kufungwa bao 1-0 ambalo lilikuwa ni la kujifunga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa wachezaji walijituma na waliweza kuhimili mikikimikiki ya wapinzani wao mwisho wa siku wakashindwa kupata matokeo.

"Mchezo wetu ulikuwa mgumu na kwa kiasi kikubwa wachezaji wangu walijituma na kufuata maelekezo kwa hilo ninawapongeza ila kwa kukosa matokeo ni sehemu ya mchezo, ligi bado inaendelea nasi tunajipanga zaidi," amesema.

Salum Yasin wa Polisi Tanzania alijifunga bao dakika ya tano ambalo lilidumu mpaka dakika ya 90 na kuipa Ruvu Shooting pointi tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic