September 15, 2019


BEKI wa zamani wa Manchester City, Vincent Kompany amesema kuwa Virgil Van Dijk ndiye beki bora kuwahi kucheza Premier League.

Dijk mwenye umri wa miaka 28 amekuwa beki bora ndani ya Liverpool tangu atue akitokea Southampton kwa dau la pauni milioni 75 katika dirisha dogo la usajili wa januari 2018.

Ana Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya akiwapiga chini Lionel Messi na Cr 7 ikiwa ni baada ya kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.


 "Sijataka kulinganisha, safari yangu ilikuwa tofauti, kwangu Dijk hana muda mrefu kwenye ligi kama ilivyo kwa John Terry na Ferdinand lakini kwa alichofanya msimu uliopita inanifanya nimuone Bora," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic