BEKI Mkongwe
ndani ya timu ya Simba, Erasto Nyoni amesema kuwa kwa sasa Simba inapitia
kipindi kigumu kutokana na kumkosa nahodha wao John Bocco kwenye majukumu ya
kazi.
Bocco anapambana
kurejea kwenye ubora wake kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata kwenye
mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, alikosa michezo miwili ya ushindani
ambo ni dhidi ya JKT Tanzania na Mtibwa Sugar.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Nyoni amesema kuwa kukosekana kwa nahodha huyo kunapunguza
ule utamu kamili wa Simba kutokana na uwezo wa uongozi alionao Bocco.
“Tunajua
kwamba Simba ina wachezaji wengi ila kila mmoja ana umuhimu wake, kukosekana
kwa Bocco kuna kitu kinakosekana pia ndani ya timu ukizingatia yeye ni nahodha
mkuu kwa sasa tunamuombea apone arejee kwenye ubora wake,” amesema Nyoni.
Kocha wa
Viungo wa Simba, Adel Zraine amesema kuwa mashabiki wasiwe
na mashaka Bocco atarejea kwenye ligi baada muda si mrefu kuanzia sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment