September 16, 2019


BONDIA Tony Rashid ambaye mwezi uliopita alifanikiwa kushinda ubingwa wa Afrika Mashariki na kati dhidi ya Haidari Mchanjo katika pambano ambalo lilifanyika club 361, Mwenge likiwa chini ya udhamini wa Globat Tv na gazeti la Championi jana ameshinda ubingwa wa Abu.

Pambano hilo lililofanyika nchini Afrika Kusini lilikuwa na ushindani naye alishinda kwa TKO raundi ya 11 akimshinda mpinzani wake wa Afrika Kusini.

Rashid amesema kuwa maandalizi mazuri yalimbebba kwenye pambano hilo na kumpa nafasi ya kuibuka na ubingwa huo.

"Nilijipanga na kufanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya pambano, shukrani kwa mashabiki kwa sapoti pamoja na jamaa wote ambao nipo nao.


"Natarajia kurejea leo majira ya saa 11:00 jioni ningependa mashabiki wajitokeze kuupokea ubingwa wao ambao nimeupata," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic