September 16, 2019


ARSENE Wenger, Kocha wa zamani wa Arsenal amewatoa Manchester United kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Premier League akidai kuwa ina 'watoto' wengi ambao bado hawajakomaa.

Raia huyo wa Ufaransa amesema United ina kikosi cha vijana anaona watapata tabu kupata mafanikio kama ilivyokuwa kwa nguli David Beckham, Ryan Giggs.

Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer ameonyesha kuwa na imani na vijana na kuamua kuachana na wazoefu kadhaa wakiwemo Lukaku na Alexis Sanchez.

Wenger ameeleza kuwa anaamini ukubwa wa timu ni mzigo mkubwa walionao vijana hao hawataweza kuwa na mafanikio ya muda mfupi. 


"Ukiicheki United ni mfano wa timu ambayo ina mpango fulani, lakini bado hawajaipata njia wanayoitaka labda hao wachezaji wao hawajakomaa kuweza kucheza kama timu ya United ndiyo maana wakicheza wanakosa nguvu ya kupambana kama timu na kuwania ubingwa," amesema.

Chipukizi wa United ni kama Angel Homes, Mason Greenwood na Daniel James aliyesajiliwa akitokea Swansea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic