September 19, 2019


Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema juzi amekutana na ujumbe kwenye simu yake wa mtu aliyejiita Hassan Dalali akiahidi kumtumia fedha za mchango wa kumpa pole baada ya kufanyiwa matibabu hivi karibuni kufuatia kusumbuliwa na homa kwa muda mrefu.

Akilimali amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari uliomfanya kwenda Muhimbili kufanyiwa vipimo na kisha kufanyiwa operesheni ndogo tumboni.

Akilimali ambaye alilipiwa deni la matibabu yake na Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameeleza mtu huyo aliamua kutumia namba iliyoonesha jina ambalo si la Dalali halisi ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba.

Mjumbe huyo ambaye amekuwa kwenye mvutano na wanachama wengi wa Yanga juu ya suala la mabadiliko ndani ya klabu hiyo, amesema ujumbe huo alioupokea juzi na ukimuahidi kuwa atapokea kiasi cha shilingi 20,000 lakini hakutumiwa chochote.

"Kuna ujumbe uliingia katika simu yangu kutoka kwa mtu aliyejiita Hassan Dalali ukisema nitapokea elfu ishirini baadaye, lakini wala hakuweza kutuma.

"Namba hiyo nilikuja kuigundua kuwa si ya Dalali ninayemfahamu baada ya kuitazama kupitia miamala ya pesa na kuonesha jina tofauti," alisema Akilimali.

Aidha, Akilimali ameeleza kuwa idadi ya michango anayopokea hivi sasa imepungua tofauti na mwanzo, huku akiomba watu wazidi kumchangia aweze kupata nauli, kwasababu bado ana ratiba ya kwenda hospitali kwa ajili ya kutazamwa na daktari.

"Bado nina ratiba ya kwenda hospitalini kwa ajili ya kuonana na daktari, hivyo inanihitaji kutumia nauli, kama watu bado wanaguswa na tatizo langu ni vema wakazidi kunichangia sababu gharama zinakuwa kubwa.

"Nawaomba mnipe msaada wenu hata kwa kidogo ambacho mtakuwa nacho kiweze kunisaidia, kwa siku natumia shilingi 15,000 kwenda Muhimbili," alisema Akilimali.

Unaweza kumchangia mzee Akilimali kupitia namba za simu ambazo ni 0658 668 819 pia 0754 668 819 jina ni IBRAHIM OMARY AKILIMALI.
ENDS

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic