MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kikosi kwa sasa kipo sawa kuimaliza Zesco kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Septemba 27 nchini Zambia.
Yanga ililazimisha sare kwenye mchezo wa hatua ya kwanza dhidi ya Zesco kwa kufungana bao 1-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.
Zahera amesema kuwa wametambua makosa yalipojificha jambo linalowapa matumaini ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa marudio.
"Tupo sawa kwa sasa tulikuwa na mchezo dhidi ya Mbeya City umetolewa kwa ajili ya kujiaanda na mchezo wetu dhidi ya Zesco hivyo nafasi yetu ya kufanya vizuri ni kubwa.
"Kila kitu kwenye mpira kinawezekana kikubwa ni sapoti ya mashabiki ili kuona ni namna gani tunaweza kufikia malengo yetu hakuna haja ya kuwa na mashaka," amesema.
mnafiki hivi kumbe anajua kuwa timu ikipata muda wa kutosha kujiandaa na mechi kama hiyo ya kimataifa inakuwa katika nafasi ya kufanya vizuri..Kwa nini Zahera ndiye aliyekuwa kiongozi wa kupinga viporo vya Simba mwaka jana..Sisi tulitegemea Zahera akisema kiporo cha Mbeya City sio sawa! au angeitumia mechi hiyo kujipima na kujiandaa na Zesco...Mbeya ni karibu na Zambia angetumia hiyo mechi kujiandaa.Je kwa namna viporo vilivyoanza sasa na ni ruhusa ikitokea amefuzu makundi si atakuwa na viporo kama vya Simba!
ReplyDeleteSimba alivunja record ya mwaka, viporo 14! Ni ngumu sana kuikuta mahali pengine popote. Maoni tutoayo yalenge kulisaidia soka la Tanzania, vinginevyo kuangalia Usimba na Uyanga utalididimiza soka letu bila kuangalia kitu gani chafaa kuboreshwa
DeleteZesco 2 Yanga 0 mechi ya marudiano Ndola September 28, 2019
ReplyDelete