September 29, 2019




AISHI Manula, mlinda mlango namba moja wa Simba msimu huu ametibua rekodi yake aliyoiweka msimu uliopita wa mwaka 2018/19 kwa kuruhusu kutunguliwa kwenye mechi za mwanzo.

Manula msimu uliopita akiwa langoni hakuruhusu nyavu kutingishwa kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons ambapo Simba ilishinda kwa bao 1-0.

Mchezo wa pili ilikuwa dhidi ya Mbeya City na Simba ilishinda mabao 2-0 kabla ya kulazimisha sare ya 0-0 na Ndanda FC, Uwanja wa Nangandwa Sijaona.

Msimu huu, Manula amenyooshwa na JKT Tanzania ambapo Simba ilishinda mabao 3-1 akatunguliwa na Mtibwa Sugar wakati Simba ilishinda mabao 2-1 na mkononi ana clean sheet moja aliyoipata mbele ya Kagera Sugar wakati Simba ikiibuka na Ushindi wa mabao 3-0.

2 COMMENTS:

  1. Waandishi Saleh Jembe tafadhali tuandikieni habari yenye kichwa
    "DAA HILI BALAA YANGA IMEJIONDOA YENYEWE!, WAMETIBUA REKODI YAO!

    hebu muwe mnaandika habari zilizo na maana au umuhimu..Mbona sasa hamjaandika Yanga imeweka rekodi kwa kuwa timu ya kwanza kujiondoa kwenye mashindano ya klabu bingwa CAF. Ndiyo ukweli huo kwa sababu bao lililoiondosha Yanga wamejifunga wenyewe..Tuandikieni hiyo habari.

    ReplyDelete
  2. Cha muhimu msimu huu Simba imeanza kwa mafanikio Makubwa mapema na Manula akiwa na kiwa go cha hali ya juu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic