KMC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Jackson Mayanja kwenye jumla ya michezo mitatu iliyocheza imefunga bao moja na kukusanya pointi tatu.
Imefungwa jumla ya mabao matatu na imepoteza michezo miwili huku ikishinda mchezo mmoja.
Ilianza kufungwa bao 1-0 mbele ya Azam FC ikiwa nyumbani Uwanja wa Uhuru, ikanyooshwa mabao 2-0 mbele ya Coastal Union uwanja wa Mkwakwani na ilishinda bao 1-0 mbele ya Namungo Uwanja wa Chamazi.
Leo inatupa kete yake ya nne mbele ya Ndanda FC, Uwanja wa Chamazi Complex.
0 COMMENTS:
Post a Comment