EXCLUSIVE: SWEDI NKWABI AJIVUA UONGOZI SIMBA
Uongozi wa klabu ya Simba unatoa taarifa kwa wanachama, mashabiki na wananchi wote kwamba Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi kwa uamuzi wake mwenyewe amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti.
Katika barua ambayo Swedi ameiandikia Bodi ya Wakurugenzi kupitia Mwenyekiti wa Bodi amesema sababu kuu ya kijiuzulu nafasi hiyo ni kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi.
Bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti ya Simba inamtakia kila la heri katika shughuli zake, na tunatumaini kwamba ataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali kabla kupata nafasi hiyo.
Utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya tutawatangazia hapo baadae.
0 COMMENTS:
Post a Comment