September 14, 2019



PATRICK Aussems, Kocha pekee Bongo raia wa Ubelgiji amesema kuwa Yanga na Azam FC zinatakiwa kuutumia uwanja wa nyumbani kupata matokeo kwenye michezo ya kimataifa kabla ya kwenda ugenini ambako huko kuna shida kubwa.

Msimu uliopita Simba ilitinga hatua ya robo fainali michuano ya kimataifa kwa kushinda mechi zake zote za nyumbani kabla ya kutolewa na TP Mazembe baada ya kulazimisha sare kwenye mchezo wa kwanza nyumbani.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems amesema kuwa anatambua kwamba Yanga na Azam FC zina kazi kimataifa wanachotakiwa kufanya ni kutumia vema uwanja wa nyumbani.

“Unajua michuano ya kimataifa nimeona namna ushindani wake ulivyo kila timu inapambana kupata matokeo nyumbani kwa kuwa kuna nguvu ya mashabiki na hakuna presha kubwa hicho ndicho ninachoamini kitafanyika kwa wawakilishi waliopo kimataifa.

“Muda wa kufuatilia kwa kweli wenzangu wanafanya nini sina kutokana na kazi yangu ndani ya Simba ila ninaamini inawezekana kwao wote Azam na Yanga kushinda,” amesema. 

2 COMMENTS:

  1. Wao wenyewe wameshindwa kuutumia uwanja wa nyumbani sasa watafundishaje wengine?

    ReplyDelete
  2. kweli wao wangeonesha mfano na ushindi popote pale mana uktegemea sana nyumban unakuwa dhaifu na unashndwa kupata ushnd ugenini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic