September 16, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kilichoiponza timu yake kulamisha sare mbele ya Zesco United ni uchu wa wachezaji wake kutafuta magoli mengi zaidi.

Yanga juzi ililazimisha sare yakufungana bao 1-1 na Zesco United mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa licha ya kuanza kufunga bao dakika ya 25 kupitia kwa Patrick Sibomana.

Zahera amesema:"Baada ya kufunga goli wachezaji wangu wakaongeza juhudi kushambulia, namna ambavyo tulikuwa tunatafuta nafasi na wenzetu pia walikuwa wanatafuta mwisho wa siku tumeambulia Sare.

"Kwa sasa tuna kazi moja mkononi kwenda kutafuta ushindi ugenini itakuwa kazi ngumu ila inawezekana kupenya kikubwa ni maandalizi na sapoti ya mashabiki," amesema.

Bao la kusawazisha kwa Zesco lilipachikwa dakika za lala salama na kiungo wa zamani wa Yanga, Thaban Kamusoko aliyeacha ganzi kwa mashabiki wa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic