LIONEL Messi nyota wa Barcelona anaona kuwa klabu yake haikufanya jitihada kubwa kumpata nyota wao wa zamani, Neymar Jr kutoka PSG.
Mazungumzo baina ya PSG na Barcelona yalifanyika kwa muda mrefu kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo ambaye alionyesha nia ya wazi ya kutaka kutimka PSG .
"Ningefurahi kuona kama Neymar Jr angejiunga nasi, binafsi sijui kama Barcelona walifanya juhudi ya kutosha kumrejesha hapa au la, japokuwa mazungumzo hayakuwa kwa rahisi kiasi hicho.
"Sikushauri wala sikuwaambia viongozi wafanye usajili kwa nyota huyo ila ninachojua mimi kulikuwa na uhitaji na kama wangempata ingekuwa ni sawa lakini kwa kuwa walikuwa na mazungumzo wao wenyewe wanajua," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment