Kocha Mkuu wa Zesco, George Lwandamina amesema alianza kujipanga na dakika za nyongeza baada ya kuona kuna ugumu wa kuifunga Yanga ndani ya dakika 90.
"Hakukuwa na nafasi ya kushinda kutokana na mabadiliko ya kikosi cha Yanga, ilicheza vizuri na ushindani ulikuwa mkubwa hivyo hesabu zangu niliamini tutakwenda muda wa nyongeza," amesema.
Yanga imeng'olewa na Zesco katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa kwa mabao 2-1, bao la pili ikiwa imejifunga kupitia kwa kiungo wake mkabaji Abdulaziz Makame aliyekuwa akipambana kuokoa.
Kwa sasa nguvu za Yanga zinaelekezwa kwenye Kombe la Shirikisho.
Kupigwa kapigwa Yanga eti halafu Zesco alibanwa?
ReplyDeleteSoma vizuri sheria za caf mwandishi hakuna dakika za nyongeza mechi ingeisha l-1 matuta
ReplyDelete