September 17, 2019


Aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi na mchezaji wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kutoitwa kwa Aishi Manula katika kikosi cha Taif Stars na Kaimu Kocha, Ettiene Ndayiragije kwake ni maamuzi sahihi.

Julio amefunguka akieleza ni maamuzi sahihi kwa Kocha Ndayiragije kuacha kumuita Manla sababu ya uzoefu.

Ameeleza kuwa Manula amekuwa hana uzoefu mkubwa sawa na Kaseja katika mashindano yote.

Julio ambaye ameachana na kazi ya kufundisha soka kwa muda, ameeleza kuwa Manul anapaswa kujifunza kwa Kaseja kwa namna ambayo amepambana mpaka kufikia hapo alipo.

"Unajua Kaseja ana uzoefu mkubwa kuliko Manula, kwangu Manula kuachwa Stars ni maamuzi sahihi kwa Kocha.

"Anapaswa kukaa chinina kujitafakari amekosea wapi na pia ajifunze kutoka kwa KAseja namna alivyopambana mpaka kufika hapo alipo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic